Home news RASMI….MAYELE NA KAGERE WAINGIA KWENYE VITA YA KUFA MTU…ATAKAYEZEMBEA KUENDA NA MAJI…ISHU...

RASMI….MAYELE NA KAGERE WAINGIA KWENYE VITA YA KUFA MTU…ATAKAYEZEMBEA KUENDA NA MAJI…ISHU IKO HIVI…


LIGI Kuu Bara imesimama kwa muda na inatarajiwa kurejea wikiendi ijayo kwa michezo miwili itakayozikutanisha Polisi Tanzania dhidi ya Kagera Sugar na ule wa Geita Gold watakaoikaribisha Coastal Union mjini Geita.

Lakini sasa ligi hiyo ikirejea ili kukamilisha mechi za raundi ya 15 za kufungia duru la kwanza, kuna vita kubwa ya ufungaji wa kati ya wachezaji wazawa na wageni, pia mapro wa kigeni wakiwa na vita yao wenyewe kwa wenyewe.

Ndio, kwa sasa kwenye orodha wa wafungaji, Reliants Lusajo wa Namungo FC anaongoza kwa mabao tisa, akifuatiwa kwa mbali Fiston Mayele wa Yanga, George Mpole wa Geita na Vitalis Mayanga wa Polisi ambao kila mmoja ana mabao sita.

Nyuma ya kina Mayele kuna Meddie Kagere wa Simba mwenye mabao matano sawa na Jeremiah Juma wa Tanzania Prisons kuonyesha msimu huu kwenye vita ya mabao kazi ipo kwelikweli.

Ukiachana na vita ya wazawa na wageni, huku Lusajo akiongoza jahazi kuna vita nyingine ya mapro wa kigeni wakiongozwa na Mayele ambao anapambana kuzima ufalme wa Kagere aliyouweka kwa misimu mitatu mfululizo iliyopita katika ligi.

Kagere ndiye mchezaji wa kigeni mwenye mabao mengi katika ligi kwa miaka ya karibuni akiwa ametumia misimu minne mfululizo kufunga 63, lakini msimu huu ana kazi ya kuchuana na Mayele aliyesajiliwa msimu huu kutoka DR Congo.

Kwa misimu miwili ya 2018-2019 na 2019-2020, Kagere ndiye aliyekuwa Mfungaji Bora kabla ya msimu uliopita wa 2020-2021 kuporwa ufalme na John Bocco ambaye ameanza simu na ukame wa aina yake katika ligi hiyo.

Bocco aliyefunga mabao 16 msimu uliopita na kuwapiku Chris Mugalu na Kagere wote akicheza nao Simba, hajafunga bao katika Ligi tangu Julai 18 mwaka jana alipotupia kambani mkwaju wa penalti wakati Simba ikiishindilia Namungo 4-0.

Ukihesabu tangu Julai 18, 2021 hadi leo ikiwa Februari 13 ni miezi sita na wiki tatu na siku tano au sawa na jumla ya siku 210 au saa 5,040.

SOMA NA HII  SIMBA YAIFANYIA UMAFIA WYDAD... BECHI LA UFUNDI LAKIRI JAMBO HILI

Achana na Bocco, turejee kwa Mayele na Kagere, nyota hao ambao timu zao zinachuana pia katika mbio za ubingwa, wanachuana kuweka heshima zao mbali na kutaka kuwabeba wenzao wa kigeni kwenye vita ya kuwania tuzo ya ufungaji.

Kama hujui ni kwamba hadi sasa ligi ikiwa imesimama zimechezwa jumla ya mechi 113, huku yakifungwa mabao 218, yakiwamo 10 ya kujifunga na mengine 154 yakifungwa na wazawa 81, huku wageni 28 wametupia 54 hadi sasa.

Katika mabao hayo 54, Mayele ndiye kinara kwa wageni akifuatiwa na Kagere huku Saido Ntibazonkiza wa Yanga na Rogders Kola wa Azam wakiwa nyuma yao na mabao manne kila mmoja.

Orodha ya wafungaji wa kigeni inawagusa pia Jesus Moloko na Khalid Aucho wote wa Yanga wenye mabao matatu kila moja kama Charles Zulu na Idris Mbombo wa Azam, huku Bigirimana Blaise na Obrey Chirwa wote wa Namungo, Ambrose Awio na Collins Opare wote wa Biashara Utd kila mmoja ametupia mabao mawili.