News

KUELEKEA MECHI YA KESHO…BOCCO AVUNJA UKIMYA SIMBA…AFUNGUKA HALI YA TIMU ILIVYO..ATAJA FITNA…

admin February 19, 2022 6:11 am


NAHODHA wa Simba, John Bocco ametaja mambo mawili yatakayowabeba kuelekea mchezo wao wa Jumapili dhidi ya USGN huko Niger.

Simba wameanza vizuri mechi ya kwanza nyumbani baada ya kuinyuka Asec Mimosas mabao 3-1 mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Mkapa.

Bocco alisema kwanza wanaenda kucheza mchezo huo wakiwa na matokeo mazuri mchezo wa kwanza na wananyota wengi wenye uzoefu na mashindano ya kimataifa.

“Ubora wa Simba kwa sasa ni mkubwa wachezaji tupo kwenye hari nzuri ya ushindani baada ya matokeo mazuri nyumbani tunatambua kuna fitna ugenini wengi ni wazoefu hatuna hofu na hizo fitna,” alisema na kuongeza;

“Tunaomba watanzania watuombee tunaenda kuiwakilisha nchi na sio Simba pekee tumejiandaa vizuri tunaenda kupambana na kutafuta furaha ya watanzania,”.

WAKATI WATU WAKIMUIMBA SAIDO…ALLY MAYAY AIBUKA NA HILI…AKOSOA UCHEZAJI WAKE…NABI APEWA ONYO… PAMOJA NA KURUDISHWA KUNDINI…MORRISON APEWA MECHI MBILI TU …LASIVYO KUTEMWA MAZIMA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply