Home news WAKATI WATU WAKIMUIMBA SAIDO…ALLY MAYAY AIBUKA NA HILI…AKOSOA UCHEZAJI WAKE…NABI APEWA ONYO…

WAKATI WATU WAKIMUIMBA SAIDO…ALLY MAYAY AIBUKA NA HILI…AKOSOA UCHEZAJI WAKE…NABI APEWA ONYO…


KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi ametonywa mapema kuhakikisha anafanya kazi ya ziada kwenye kuboresha upigaji wa mipira iliyokufa ili kupata mabao mengi zaidi kwenye kila mchezo.

Jambo hilo lilitokana na mchezo wao wa 16 bora kwenye Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) dhidi ya Biashara United kupata nafasi nyingi za mipira ya kona na frii-kiki lakini walishindwa kuzitumia ipasavyo.

Winga wake Saido Ntibazonkiza ndiye aliyekuwa anahusika kwenye kupiga mipira hiyo kwenye mchezo huo lakini hakuwa kwenye kiwango kizuri akishindwa kutumia mipira hiyo ya adhabu.

Katika kona 11 ambazo walipata kwenye mchezo mzima huku Biashara Utd wakipata kona moja tena kwenye kipindi cha pili, Ntibazonkiza alipiga kona zote huku moja tu ya dakika 21 ndiyo ilizaa bao la kwanza alilofunga Yanick Bangala ambalo lilitokana na kipa kuutema mpira kisha yeye alipiga krosi tena na kupigwa kichwa na Bakari Mwamnyeto na kugonga mwamba kisha Yanick Bangala alipiga kichwa ukachezwa na kipa wa Biashara na ulipotua chini Mcongo huyo aliupiga na kwenda wavuni.

Saido pia alipiga frii-kiki kadhaa ikiwamo ya dakika 45 baada ya kiungo Khalid Aucho kufanyiwa madhambi nje kidogo ya boksi lakini akapaisha, na alikosa pia frii-kiki nyingine nje ya boksi katika dakika 62 baada ya yeye mwenyewe kuangushwa nje kidogo ya boksi.

Licha ya kukosa ‘frii-kiki’ nyingi na kupiga kona ambazo hazikuzaa mabao, Ntibazonkiza alihusika kwenye bao la pili dakika 29 baada ya kuwatoka mabeki wa Biashara United na kupiga pasi kwa Fiston Mayele aliyeuweka mpira wavuni.

WADAU WAFUNGUKA

Mshambuliaji wa zamani Yanga, Hery Morris alisema wapigaji wanatakiwa wapatikane wawili au watatu ili mmoja asipokuwa kwenye siku nzuri basi mwingine apige.

“Ilikataa jana kwa Ntibazonkiza, kiukweli niliangalia na kila mpira aliokuwa anapiga unapaa licha ya huko nyuma alikuwa anafunga, benchi la Yanga halikuelewa mapema kama mchezaji hayupo kwenye siku nzuri,” alisema Morris.

Upande wa Ally Mayay ambaye ni mchambuzi wa soka, alisema kitu pekee ambacho kinaonyesha ubora wa mazoezi ni mechi na upande wa Ntibazonkiza ulikuwa ni urudiaji wa makosa ya mara kwa mara.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMAPILI

“Urudiaji wa makosa ni tatizo kwa sababu hivi vitu vinafanyika kwenye mazoezi na ukiwa bora unakuja kufanya kwenye mechi, Saido hakuwa kwenye ubora katika kona na hata frii-kiki,” alisema Mayay na kuongeza;

“Frii-kiki sio zote unaweza kupiga mtu mmoja kwa sababu kuna frii-kiki inatakiwa ipigwe na anayetumia mguu wa kulia na mwingine mguu wa kushoto.”

Mayay alienda mbali zaidi na kusema timu za Misri zikipata mipira ya adhabu huwa ni neema kwao kwa sababu huwa wanajua namna ya kuitumia na kupata mabao.

“Mfano tosha Al Ahly ya Misri kwenye mipira mitatu ya frii-kiki hawawezi kukuacha salama.”