news

BAADA YA KUSIKIA TAMBO ZA BANDA NA MTIBWA YAKE…MAYELE AGUNA KISHA AKASEMA HAYA…

admin February 22, 2022 12:46 pm


MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Mayele, ameapa kuipambania Yanga katika mchezo unaofuata wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar kwa kuhakikisha timu hiyo inaibuka na ushindi wakiwa ugenini.

Yanga katika mchezo huo, wanatarajiwa kuwa ugenini kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro, utakaochezwa keshokutwa Jumatano.

 Mayele alisema kuwa licha ya kufahamu kuwa mchezo huo utakuwa mgumu lakini watapambana kama timu kuhakikisha wanaibuka na ushindi muhimu katika mchezo huo kutokana na kufahamu umuhimu wa mchezo wenyewe.

“Tunafahamu ukubwa wa mchezo huu, ni mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa ligi, hivyo tunatakiwa kuumaliza kwa ushindi, naona utakuwa mchezo mgumu kwa kuwa tutakuwa ugenini lakini hatuhofii hilo.

“Sisi tupo tayari kwa ajili ya mapambano na tutapambana mpaka dakika ya mwisho kuhakikisha tunaondoka na ushindi, kila mchezo kwetu unahitaji ushindi, na hiyo ni kutokana na kuhitaji kutimiza malengo yetu msimu huu,” alisema Mayele.

KUELEKEA MECHI NA MTIBWA…YANGA WAPATA PIGO…MOLOKO KUPIGWA KISU..WATANO WANAUGULIA … SHABANI DJUMA ARUDISHA AMANI YANGA…’SURE BOY’ MGUU NDANI MGUU NNJE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply