Home news SIMBA WATUA MOROCCO KITAJIRI…BERKANE WAPIGWA BUTWAA…BARBARA AONGOZA UJASUSI…

SIMBA WATUA MOROCCO KITAJIRI…BERKANE WAPIGWA BUTWAA…BARBARA AONGOZA UJASUSI…


RS Berkane ya Tuisila Kisinda na Kocha wake Florent Ibenge imerejea Morocco ikiwa na maumivu ya kipigo cha mabao 3-1 walichopewa na Asec Memosasya Ivory Coast.

Lakini wamepigwa na mshtuko baada ya kukutana mtaani na vigogo wa Simba ambao tayari walishatua Morocco kufanya yao.

Berkane na Simba watakiwasha Jumapili kwenye mechi ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Viongozi wa Simba tayari wapo Morocco kwa ajili ya maandalizi muhimu baada ya kupata sare ya bao 1-1 na USGN nchini Niger juzi usiku na wamesisitiza kwamba kila kitu kipo kwenye mstari.

Inafahamika kuwa msafara wa viongozi wa Simba ulishatua muda chini ya Ofisa mtendaji mkuu, Barbara Gonzalez lakini timu ilitua jana Morocco baada ya kutoka kambini Niger.

Barbara ambaye ni mzoefu wa Morocco alisema alitangulia kwa ajili ya kuhakikisha timu inafikia kwenye hoteli nzuri pamoja na kutumia vitu muhimu wao wenyewe kwani wana uzoefu na michuano hiyo na wanajua cha kufanya.

“Ni utaratibu wetu kabla ya timu kufika lazima kutakuwa na kundi la kwanza limetangulia kuandaa mazingira muhimu na Morocco ndio tumefanya hivyo kikubwa tunafanya yote haya kwa ajili ya kupata matokeo mazuri,” alisema Barbara na kuongeza:

“Bado maamuzi ya timu itafika Morocco lini hayajafanyika ila kuna vitu vya msingi vikikamilika watakuja.”

PABLO AFUNGUKA

Kocha wa Simba, Pablo Franco amesema kwenye Kombe la Shirikisho Afrika ni ngumu mno kupata pointi ugenini kama ambavyo wachezaji wake wamefanya katika mchezo wa USGN uliopigwa juzi Niger.

Pablo alisema mechi ilikuwa ngumu kwenye maandalizi kutokana na kukosa muda wa kutosha wa kufanya mazoezi tangu walipocheza mchezo wa mwisho ikiwemo umbali wa kusafiri kwa muda mrefu.

Alisema katika maandalizi walikutana na ugumu mwingine wa kuwakosa wachezaji wake muhimu kama Jonas Mkude na Israel Mwenda ambao wanaumwa.

“Ilikuwa siri kubwa kwani kuna wachezaji wengine walilazimika kucheza huku wakiwa hawapo fiti kwa asilimia zote jambo ambalo ukiangalia hata katika benchi letu la akiba kulikuwa na makipa wawili Ally Salim na Benno Kakolanya,” alisema Pablo.

SOMA NA HII  ZORAN : NATAKA KUFIKA MBALI NA SIMBA....YANGA NAIJUA KIDOGO SANA...NINGEPEWA MIAKA MINNE INGEKUWA POA SANA...

Katika hatua nyingine Pablo alisema pointi waliyopata ugenini ina maana kubwa kwao kwani imewaongezea morali na kila mchezaji anatamani kufanya hivyo hata katika mchezo unaofuata ugenini utakuwa dhidi ya RS Berkane.

Kiungo wa Simba, Clatous Chama ambaye hakutumika katika mechi hiyo alisema; “Haikuwa kazi rahisi kutanguliwa bao na timu mwenyeji ila wachezaji wote waliopata nafasi ya kucheza walihakikisha tunasawazisha na ilikuwa hivyo si mbaya ni mwanzo mzuri kwetu.”

KUJENGWA KISAIKOLOJIA

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah ‘Try Again’ alisema watakaa na nyota wao ili kuwajenga kisaikolojia kuelekea mchezo ujao.

“Tunakaa na wachezaji wetu na kuzungumza nao wapambane, wakae wakijua kila mchezo kwetu ni fainali hivyo tunahitaji matokeo,” alisema huku akiisitiza kuwa michuano hiyo ni migumu na kila timu inapambana kuhakikisha inapata matokeo katika uwanja wa nyumbani.

“Mchezo wa Niger tulimuomba Mungu atusaidie tupate hata pointi moja kama tatu zikishindikana na tulipata moja, sio jambo dogo kupata alama ugenini ni jambo la kujivunia na kuwapongeza wachezaji wetu,” alisema Try Again huku akisisita mashabiki kuendelea kuwasapoti wachezaji wao.