news

MASOUD DJUMA AANZA KWA MKWARA MZITO DODOMA JIJI…AWAKIMBIZA WACHEZAJI MCHAKAMCHAKA JUANI…

admin February 25, 2022 8:52 am


Kocha mpya wa timu ya Dodoma Jiji Masoud Jumaa ameanza rasmi kibarua cha kukinoa kikosi cha timu hiyo jana katika uwanja wa Jamhuri jijini hapa.

Masoud anachukua nafasi ya Mbwana Makata ambaye hivi karibuni amefungashiwa virago na uongozi wa timu hiyo sababu zikitajwa ni kutoridhishwa na matokeo ya timu hiyo.

Katika mazoezi ya jana yaliyoanza majira ya saa 10 jioni Kocha huyo alianza kwa  kutambulishwa kwa wachezaji na uongozi wa timu hiyo na kisha kuanza mazoezi ya mbio.

Akiwa na kocha Msaidizi Mohammed Muya,Jumaa alionekana kusisitizia mazoezi ya kutafuta pumzi ambapo muda wote alikuwa akibadilisha Koni na wachezaji wakikimbia katika koni hizo.

BAADA YA KUSIKIA ‘KAZI CHAFU’ ZA SAKHO NA MORRISON..IBENGE AKUNA KICHWA WEE..KISHA AKASEMA KUNA SHIDA… TFF YAWAPIGIA MAGOTI GSM…WARUDI MEZANI UPYA KUJADILI DILI..MGUTO ATUPA MPIRA KWA KIDAO..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply