news

WAKATI IBENGE NA WENZAKE WAKIHAHA …SIMBA YAPEWA SHAVU NA KLABU YA RAJA CASABLANCA YA MOROCCO..

admin February 26, 2022 5:20 am


NI jino kwa jino huko Morocco. Katika kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mchezo wao wa keshokutwa Jumapili dhidi ya RS Berkane, uongozi wa Simba umeamua kutumia uhusiano wao na maofisa wa Raja Casablanca ya Morocco kuhakikisha wanapata mbinu za kuwamaliza Berkane.

Simba inanufaika kutokana na kuwa na makubaliano ya ushirika na Klabu ya Raja Casablanca yaliyotokana na ziara ambayo aliifanya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez mwaka jana katika nchi za Morocco na Misri.

Akizungumzia mapokezi yao kutoka kwa uongozi wa Raja Casablanca ya Morocco baada ya kuwasili nchini humo, Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola, alisema: “Tunashukuru kwa kufanikiwa kufika salama hapa Morocco baada ya safari ndefu kutokea nchini Uturuki, ambapo tulikuwa na mapumziko ya muda mfupi baada ya kutokea nchini Niger.

“Jambo lililotufurahisha zaidi ni mapokezi mazuri ambayo tumeyapata kutoka kwa uongozi wa Klabu ya Raja Casablanca ya hapa ambao kwa kiasi kikubwa wameshirikiana na viongozi wetu waliotangulia hapa kuhakikisha tunafikia mahali salama na pia kupeana uzoefu juu ya wapinzani wetu na kuhakikisha tunafanya vizuri.” Simba ikiwa Morocco inatumia pia basi kubwa la Raja Casablanca katika mishe zote nchini humo.

ZAHERA AFUNGUKA KUHUSU YANGA…CHAMA AWAUZA BERKANE..IBEGE APAGAWA..AOMBA MSAADA… PAMOJA NA KUISAIDIA …AUCHO AVUNJA UKIMYA…AFUNGUKA HAYA KUHUSU YANGA…SIMBA YATAJWA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply