Home news KISA YANGA KUSHINDWA KUPATA USHINDI JUZI…SERIKALI YAPANGA KULETA VAR KWENYE LIGI YA...

KISA YANGA KUSHINDWA KUPATA USHINDI JUZI…SERIKALI YAPANGA KULETA VAR KWENYE LIGI YA BONGO…


BAADA ya matukio mengi ya soka kwa upande wa waamuzi kutokufuata sheria 17 Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba ameibuka na kutaja suruhu.

Nchemba ameibua hayo baada ya jana Yanga kunyimwa nafasi ya wazi ya kufunga bao kwa mwamuzi msaidizi kuashiria ameotea (offside).

Kupitia mtandao wake wa kijamii Instagram Nchemba amependekeza kuweka chombo kitakacho msaidia mwamuzi kurudia tukio uwanjani (VAR).

“Nitaongea na Waziri mwenzangu anayesimamia michezo bajeti ijayo tumtafutie fedha, tuweke VAR viwanja hata 10 ambayo itasaidia kupunguza makosa yaliyopo,” anaandika na kuongeza;

“Pia tuweke nyasi bandia kuondoa utaratibu wa kucheza mpira shambani, haya ndio maeneo yanayolalamikiwa sana kwenye ligi yetu,” alisema na kuongeza kuwa Yanga jana kama sio makandokando ya waamuzi ilistahili kushinda.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA WANIGERIA....EDO KUMWEMBE AIPASUKIA UKWELI YANGA...ATAJA YA TAIFA STARS...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here