Home news KUELEKEA MECHI DHIDI YA SIMBA…MKWASA AANZA KULIA MAPEMA…AMATAJA MAREHEMU SONSO…

KUELEKEA MECHI DHIDI YA SIMBA…MKWASA AANZA KULIA MAPEMA…AMATAJA MAREHEMU SONSO…


IKIWA Jumamosi iliyopita ndiyo siku ambayo beki wa zamani wa Lipuli, Yanga, Kagera Sugar na Ruvu Shooting, Ally Mtoni ‘Sonso’, alipumzishwa kwenye makazi yake ya milele, kocha wa Ruvu, Charles Mkwasa, amesema Sonso ameacha pengo kwenye kikosi chake.

Mkwasa alisema Sonso alikuwa ni mchezaji wa kutumainiwa kwenye timu hiyo na ndiyo maana hata alipoanza kuumwa alikuwa yupo kwenye mipango ya kumtumia kwenye mchezo dhidi ya Simba uliocheza jijini Mwanza, Novemba 19 na Ruvu wakapoteza 3-1.

Mkwasa alisema  kuwa: “Sonso ameacha pengo kwenye klabu yetu, kwa sababu alikuwa mchezaji muhimu kwenye timu yetu, ndiyo maana hata alipoanza kuumwa alikuwa yupo kwenye mipango ya mechi.

“Ameacha huzuni kubwa sana kwenye timu yetu, bado kuna msiba kwa sababu wachezaji wenzake wengi bado wanamlilia.”

Sonso alifariki dunia jioni ya Ijumaa ya wiki iliyopita na kuzikwa kwenye makaburi yaliyopo Magomeni jijini Dar huku chanzo cha kifo chake ikitajwa kuwa ni kidonda kwenye mguu wake.

SOMA NA HII  KOCHA MPYA SIMBA ALETA MAFUNDI WAWILI...ABADILI POSHO ZA MASTAA SIMBA...MAYELE, BANGALA WATOLEWA...