Home Uncategorized AHADI YA MORRISON KWA SIMBA IPO HIVI

AHADI YA MORRISON KWA SIMBA IPO HIVI

Mghana Bernard Morrison ambaye amesaini dili la miaka miwili Simba, amesema mashabiki wa timu yake hiyo mpya wasiwe na wasiwasi kwani hatakuwa na usumbufu kama waliouona akiwa Jangwani.

 

Mghana huyo amesema kuwa kilichomvutia kutua Simba ni ubora wa kikosi walichonacho, wakiwa na viungo Clatous Chama na Luis Miquissone, pia anataka kucheza michuano ya kimataifa msimu ujao.

 

“Kabla ya kusaini Simba niliangalia baadhi ya vitu vikiwemo suala la ubora wa kikosi cha sasa cha hapa, kitu ambacho kimenishawishi kujiunga nao kwa ajili ya kufanya nao kazi kwa msimu ujao.

 

“Lakini pia mimi kama mchezaji nina malengo yangu ya kutaka kucheza kimataifa na Simba wanayo nafasi hiyo, ndiyo maana nikaona kuna umuhimu wa kujiunga nao kwa ajili ya kuonekana zaidi msimu ujao,” aliweka nukta Mghana huyo.

 

Nyota huyo Mghana wakati akiwa Yanga anakumbukwa kutokana na matukio yake kadhaa ya utata ambapo baada ya kutua Simba amefunguka kuwa atatulia na kuwaahidi mashabiki wa klabu hiyo kutazama kile ambacho atakifanya uwanjani na kuachana na masuala yaliyopita.

 

“Mashabiki wa Simba kwa sasa wanachotakiwa kufanya ni kuangalia kile ambacho nitaenda kufanya nikiwa kwao na siyo masuala yaliyopita. Watazame kile ambacho nitaenda kukifanya nikiwa uwanjani kwa ajili ya timu yangu,” alimaliza Morrison.

SOMA NA HII  GEITA GOLD KUJA NA TAMASHA LA KUTAMBULISHA WACHEZAJI WAKE