Home news KUELEKEA MECHI NA WAMOROCCO..CHAMA AMWAGIA SIMBA SIRI ZA BERKANE..ATOA ONYO HILI…

KUELEKEA MECHI NA WAMOROCCO..CHAMA AMWAGIA SIMBA SIRI ZA BERKANE..ATOA ONYO HILI…


KIUNGO wa Simba, Clatous Chama amewaibia siri nyota wenzake wa klabu hiyo wakati wakijiandaa kucheza na RS Berkane akiwataka kuwa makini zaidi uwanjani na kucheza kwa malengo wakati wote wa mchezo huo.

Chama amesema kuwa wapinzani wao hao ni watu hatari na kwenye hatua kama hii ambapo kila timu huwa inahitaji kupata ushindi na kutimiza malengo ambayo wamejiwekea.

Chama alisema wakati wakiwa wanakwenda kucheza mechi yao dhidi ya RS Berkane wanatakiwa kuwa kuwa huru na kufurahia kila hatua ya mchezo huo kwani hiyo ndiyo njia pekee ya kuweza kufanikiwa.

“Kikubwa wanatakiwa watambue kuwa wapo juu ya msimamo na wanatakiwa kufanya kila kitu hili kuhakikisha wanabakia kwenye nafasi hiyo.

“Wafurahie mchezo na kuwa huru wakati wote wa mechi kwani hiyo ndiyo njia pekee ya kuweza kufanikiwa,” alisema.

Chama hatokuwepo kwenye mchezo huo dhidi ya RS Berkane kutokana na kubanwa na kanuni na mechi itachezwa Februari 27, nchini Morocco.

Chama aliitumikia Berkane kwa miezi sita, kabla ya kuvunja mkataba na kurejea tena Simba. Simba ni vinara wa kundi D wakiwa na pointi nne, huku Berkane na Asec Mimosas wakiwa na pointi tatu kila mmoja na US Gendermarie wakiwa na alama moja.

SOMA NA HII  KOCHA SIMBA AVUNJA UKIMYA...CHAMA,BALEKE NA TSHABALALA WATAJWA...AFUNGUKA HAYA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here