Home news MASAU BWIRE AFUNGUKA A-Z KUUMWA HADI KIFO CHA SONSO…ADAI FAMILIA WALIINGILIA KATI…AITAJA...

MASAU BWIRE AFUNGUKA A-Z KUUMWA HADI KIFO CHA SONSO…ADAI FAMILIA WALIINGILIA KATI…AITAJA SIMBA….


Huzuni na vilio vilitawala wakati mwili wa aliyekuwa mchezaji wa Ruvu Shooting, beki Ally Mtoni Sonso ulipokuwa ukiwasili nyumbani kwa wazazi wake mtaa wa Mzumbe, Magomeni Kondoa jijini Dar es Salaam.

Watu wengi waliangusha vilio wakati mwili wa beki huyo uliposhushwa kwenye gari ukitokea hospitali ya Taifa ya  Muhimbili.

Sonso alifariki Dunia jana jioni katika hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu ya mguu.

Akimuelezea marehemu, msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire alisema wamepata pigo kubwa kwani Sonso alikuwa mchezaji mwenye upendo na muhamasishaji katika timu yao.

“Tumepoteza jembe kwani moja ya sifa ya Sonso ilikuwa ni kuhamasiaha wenzake wawapo uwanjani na pia mshauri mkubwa wa wenzake nje ya uwanja pia alikuwa na upendo sana kwa wengine.

“Alianza kuumwa Novemba 19 wakati tukiwa Mwanza tukijiandaa kucheza na Simba siku hiyo huku yeye akiwa miongoni mwa wachezaji waliopangwa kucheza kikosi cha kwanza, lakini  majira ya saa tano asubuhi akamwambia kocha Charles Boniface Mkwasa kuwa anajisikia maumivu katika mguu wa kushoto na kocha akamuelekeza kumuona daktari wa timu ambaye alimpa dawa ya kutuliza maumivu.

” Majira ya saa saba mchana wakati tunajiandaa kutoka kuelekea uwanjani akamfata tena kocha na daktari akawaambia bado maumivu yanazidi na mguu unaanza kuvimba ndipo akaondolewa kwenye ratiba ya mechi hiyo, ” amesema Masau na kuongeza

“Tuliporudi Dar es Saalam madaktari wetu walimshauri abakie kambini ili kupata matibabu zaidi na alikubali na siku kadhaa baadae aliondoka na kurejea nyumbani kwake Chamazi.

” Hata hivyo Desemba Mosi  walipata taarifa kuwa hali ya Sonso sio nzuri hivyo wanahitaji msaada wa matibabu ndipo  mwenyekiti wa Ruvu Shooting Kanali Peter Elias Mnyali akatuamuru kwenda kumfata na kumpeleka hospitali ndipo kesho yake tukamfuata alfajiri na gari ya kubebea wagonjwa na kumpeleka hospitali ya Taifa Muhimbili.,” Amesema Bwire.

Bwire alisema baada ya kufika Muhimbili  na kukamilisha taratibu zote kwa ajili ya kupata matibabu familia yake na yeye mwenyewe wakiomba wasitibiwe hapo na wanataka kwenda sehemu nyingine ambayo waliona watapata matibabu zaidi.

SOMA NA HII  SAMATTA KUMBE UMRI TATIZO

“Baada ya kushauriana tukaona tukubali maana familia ndio imeamua na ndipo wakaondoka nae hadi tulipopata taarifa jana jioni kuwa amefariki. Mungu ampumzishe kwa amani ,” amesema Bwire.