Home news MORRISON ALIVURUGA SIMBA…ISHU YAKE YA KURUDI TENA YANGA IKO HIVI KUMBE..AFUNGUKA HILI…

MORRISON ALIVURUGA SIMBA…ISHU YAKE YA KURUDI TENA YANGA IKO HIVI KUMBE..AFUNGUKA HILI…


KIUNGO mshambuliaji wa Kimataifa Raia wa Ghana, anayekipiga ndani ya Klabu ya Simba, Bernard Morrison asimamisha kwa muda hadi suala lake la kinidhamu litakapo paatiwa ufumbuzi.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya klabu hiyo, Morrison amekuwa na tabia ya kutoka kambini bila ruhusa kinyume na taratibu

Aidha ametakiwa kutoa maelezo ya maandishi kwa mtendaji mkuu wa Simba ana akishindwa kufanya hivyo hatua zaidi za kinidhamu zitachukuliwa.

Kupitia mtandao wake wa Instagram na Twitter, Morisson ameandika; “Jambo kubwa linakwenda kutokea, unaweza kuhisi ni nini???????

Hata hivyo,duru za ndani kutoka ndani ya viunga vya Yanga, vinasema kuwa kuna uwezekano mkubwa nyota huyo akarudi klabuni hapo kwa msimu ujao.

Morrison ambaye aliondoka Yanga misimu miwili iliyopita kwa ghiliba kubwa, anahusishwa kurudi tena kwenye Klabu hiyo iliyomsajili kwa mara ya kwanza akitokea nchini Afrika kusini aliokuwa anacheza soka la kulipwa kwenye klabu ya Orlando Pirates.

Hata hivyo chanzo chetu hakijweza kubainisha moja kwa moja ni mkataba wa muda gani atajiunga na klabu hio, japo inafahamika wazi kuwa huenda akasaini mkataba wa miaka miwili.

Mkataba wake na Simba unamalizika mwishoni mwa msimu huu, ambapo toka kujiunga na miamba hio ya soka nchini kutoka viunga vya msimbazi, Morrison hajakuwa na msaada mkubwa tofauti na matarajio ya wengi.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA