news

HIVI NDIVYO HENOCK INONGA ALIVYOKAMILISHA BIASHARA YAKE NA BIASHARA UTD JUZI..NI KIMYA KIMYA MZEE…

admin March 7, 2022 3:00 pm


BEKI wa Simba, Henock Inonga,Uwanja wa Mkapa alikuwa na biashara yake uwanjani mbele ya Biashara United kwenye mchezo wa ligi wakati Simba ikishinda kwa mabao 3-0.

Aliweza kutumia jumla ya dakika 65 na kutolewa kutokana na kupata maumivu lakini aliacha biashara ya msako wa pointi tatu ukiwa umekamilika kwa kuwa Simba ilikuwa tayari imeshatupia mabao hayo matatu mpaka muda anafanyiwa mabadiliko.

Alipiga jumla ya pasi 35 ambapo kwa mguu wa kulia huu ulionekana kuwa wenye nguvu kwake alitoa pasi 29 huku ule mguu wa kushoto akitoa pasi 2, alichezewa faulo 2 alipiga mipira kwa kichwa mara 4 alicheza faulo 1 alikokota mara 16 alitumia dakika 65 nafasi yake aliingia Kenned Juma.

Sababu ya kushindwa kuyeyusha dakika 90 alipata maumivu kabla mchezo haujakamilika hivyo yalikuwa ni mabadiliko ya lazima kwa Simba.

Alikuwa ni mchezaji wa pili kuweza kufanyiwa mabadiliko ya lazima kwa kuwa Pablo Franco hakuwa na chaguo dakika ya 30 alitoka beki Shomari Kapombe ambaye alipata maumivu nafasi yake ilichukuliwa na Israel Mwenda.

KUHUSU HALI YA MANULA NA MUSTAKABALI WAKE SIMBA…UONGOZI WATOA TAMKO HILI… METACHA ATAJWA KIPIGO CHA AZAM…MALALE HAMSINI ASHINDWA KUJIZUIA…AFICHUA SIRI NZIMA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply