news

PAMOJA NA KUONGOZA LIGI…NABI KAKITAZAMA KIKOSI CHAKE WEE..KISHA AKATOA OMBI HILI YANGA…

admin March 11, 2022 6:21 am


KATIKA kuhakikisha anafanya vema michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara na kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo, Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, ameiomba Kamati ya Mashindano kumpatia mchezo mmoja wa kirafiki.

Hiyo ni katika kujiweka fiti kipindi hiki ambacho Yanga haina mechi ya kimashindano hadi Machi 16, mwaka huu watakapocheza dhidi ya KMC kwenye Ligi Kuu Bara.

Lengo la mchezo huo unaotarajiwa kupigwa Jumamosi ya wiki hii ni kuangalia fitinesi ya wachezaji wake waliokuwa majeruhi akiwemo Chico Ushindi, Khalid Aucho, Shaban Djuma na Saidi Ntibazonkiza.

Nabi alisema mchezo huo wa kirafiki pia atautumia kuwapa nafasi wachezaji ambao wamekosa nafasi ya kucheza katika michezo ligi na Kombe la Shirikisho la Azam.

“Mchezaji mmoja akitumika kwa muda mrefu anachoka, hivyo ili kuhakikisha wachezaji hao hawapati uchovu, nimepanga kutengeneza mzunguko wakicheza kwa kubadilishana ili wengine wapate muda wa kupumzika.

“Kama unavyofahamu ligi ni marathoni, hivyo ni lazima kuwepo na mzunguko wa wachezaji kubadilishana katika baadhi ya michezo wakati tukiwa tunaelekea kumaliza msimu ambao ni mgumu.

“Hivyo basi ili hao wengine ambao hawakutumika kwa mfululizo katika michezo iliyopita, nitatoa nafasi kwao ya kucheza kwa kuanzia mchezo huu wa kirafiki tutakaoucheza kabla ya kucheza mchezo wetu ujao wa ligi dhidi ya KMC,” alisema Nabi.

KUIUA BERKANE…SIMBA YAPEWA NONDO NNE MATATA..LWANGA AKOLEZA MZUKA..MASTAA YANGA WAAPA… WAKATI YANGA WAKICHEZA NA WASOMALI …KMC WAONA ISIWE TABU…HITIMANA ‘AJICHONGEA RUNGU LA KUUA’

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply