news

KUELEKEA MECHI YA KESHO…ZIMBWE Jr AVUNJA UKIMYA SIMBA…AFUNGUKA KUHUSU MAPUNGUFU YAO…

admin March 12, 2022 6:00 pm


Nahodha Msaidizi Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ ameweka wazi kuwa wachezaji wapo kamili kuikabili RS Berkane katika mchezo wa kesho wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni.

Zimbwe Jr amesema makosa tuliyofanya katika mchezo uliopita nchini Morocco benchi la ufundi limeyafanyia kazi na kesho ni zamu yetu kupata ushindi.

Mlinzi huyo wa kushoto ameongeza kuwa moja ya sababu iliyotufanya kupoteza mchezo uliopita kule Morocco ni uwepo wa mashabiki ambao walikuwa wanaisapoti kwa wingi timu yao hivyo kesho itakuwa zamu yetu kupata nguvu ya mashabiki.

“Kwa upande wa wachezaji tupo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho, tunajua umuhimu wa kushinda mechi hii pia tunataka kuwapa furaha mashabiki wetu.

“Mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo wa kwanza benchi la ufundi iliyaona na tumeyafanyia kazi mazoezini. Kikubwa nawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi uwanjani kutupa sapoti tunaamini tutawapa furaha,” amesema Zimbwe Jr.

WAKATI WATU WAKIANZA KUMUELEWA…BANDA KAWATAZAMA WEE..KISHA AKASEMA HAYA…PABLO KAKOLEZA CHUMVI.. BAADA YA KUSIKIA KESHO WAARABU WANASHUSHA ‘FULL MZIKI’…PABLO KAGUNA..KISHA AKAMTAJA MZAMIRU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply