Baada ya Paul Makonda kuwalalamikia Polisi kwamba kuna baadhi ya Askari Polisi wanadhalilisha Jeshi la Polisi sababu wanatumiwa na Matajiri.
Haji Manara ambaye ni Msemaji wa Klabu ya mpira wa Miguu ya Yanga SC ya Tanzania, amesema atulie tuli kama ananyolewa.
Haji kadai Wakati Makonda akiwa Serikalini, alimlaza Korokoroni bila sababu.
Ipo hivi; Jana Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM iliyokutana Dodoma, chini ya Mwenyekiti wake Rais Samia Suluhu, imeiagiza Serikali kuchunguza mwenendo wa Jeshi la Polisi baada ya wananchi kupoteza imani na Jeshi hilo.
Inadaiwa Maofisa wa Polisi hawaaminiki na wanaonekana kutenda majukumu yao bila kufuata Mwongozo wao wa kisheria (PGO).
Baada ya taarifa hiyo, Paul Makonda Aliandika hivi;
Naunga Mkono hoja ya Kamati kuu ya kuchunguza mwenendo wa baadhi ya maafisa wa jeshi la Polisi, wanaolipaka tope jeshi la polisi kwa kuwalinda wafanyabiashara MATAPELI wanaodhurumu mali za watu.
Naomba tuanze na Dar Es Salaam na Mimi Paul Makonda nipo tayari kutoa ushirikiano.
Baada ya kuandika Ujumbe huo, Haji Manara alijibu hivi;
Mimi mwenyewe Ushawahi kuniweka ndani bila kosa kwa kutumia Polisi hao hao unao walaumu leo.
Watu wangapi uliwasweka lockup kwa kutumia cheo chako? Wewe leo wa kuwalaumu Polisi?
Acha waseme wengine na tulia Dunia iendelee kuzunguka katika mhimili wake.