Home news BAADA YA KUWACHARAZA WAARABU JUZI…PABLO AWAZA KUPATA KIBONDE ROBO FAINAL CAF…

BAADA YA KUWACHARAZA WAARABU JUZI…PABLO AWAZA KUPATA KIBONDE ROBO FAINAL CAF…


KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco, ameweka wazi kuwa hesabu zao ni kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika michezo yao iliyosalia ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, ili kumaliza kileleni mwa msimamo wa Kundi D, hali itakayowafanya wapate ahueni ya kukutana na ‘kibonde’ katika michezo ya robo fainali.

Pablo anataka kikosi chake kimalize kinara wa Kundi D, kwa kuwa kanuni za mashindano zinampa nafasi ya kinara wa kundi kukutana na timu iliyomaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi jingine, ambayo kwa kawaida inakuwa kibonde kulinganisha na zile zilizomaliza vinara kwenye makundi yao.

Simba juzi Jumapili walikuwa na kibarua cha mchezo wao wa nne wa hatua ya makundi dhidi ya RS Berkane ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam, ambapo wamesaliwa na michezo miwili tu kutamatisha hatua hiyo, ule wa ugenini dhidi ya ASEC Mimosas na wa nyumbani dhidi ya USGN.

Kocha, Pablo alisema: “Malengo yetu kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho msimu huu ni kuhakikisha tunacheza angalau nusu fainali, na katika kufanikisha hilo ni wazi tunapaswa kufanya kazi kubwa katika michezo yetu ya mwisho ili kuhakikisha tunapata matokeo.

“Tunataka kumaliza kama vinara wa kundi hili, ambapo hiyo itatusaidia kwa kiasi kikubwa kukutana na mpinzani ambaye atakuwa sio kiongozi wa kundi jingine katika hatua ya mtoano jambo litakalotupa ahueni zaidi.”

SOMA NA HII  WAKATI LEO NI MECHI YAKE YA MWISHO NA JEZI NYEKUNDU...SIMBA WAMUAGA WAWA KWA 'JIWE 'HILI DHIDI YA MTIBWA...