Habari za michezo

MSUVA AMPOTEZEA MAZIMA MAYELE….AAMUA KUWABEBA LUSAJO NA GEORGE MPOLE..

admin March 19, 2022 6:13 pm


MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva amempotezea kiaina straika wa Yanga, Fiston Mayele na kuwapigia debe George Mpole wa Geita na Reliants Lusajo wa Namungo kubeba tuzo ya Mfungaji Bora msimu huu.

Mayele ana mabao 10 sawa na Lusajo, huku Mpole akiwa nyuma yake na mabao nane, lakini Msuva aliyewahi kunyakua mara mbili Tuzo ya Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara akiwa na Yanga, alisema anatamani kuona wazawa wakitamba mbio hizo.

“Mayele ni mshambuliaji mzuri, ila natamani sana kuona mzawa akiwa mfungaji bora, ligi yetu ina wachezaji wengi wazuri wanaofanya vizuri hivyo namna pekee ya kuthibitisha hilo ni kutwaa tuzo muhimu,” alisema Msuva anayecheza soka la kulipwa Morocco japo ana mgogoro kwa sasa na klabu yake ya Wydad Casablanca.

“Kiukweli, Mpole na Lusajo wapo kwenye viwango bora na naamini mmoja wao anaweza kuwa mfungaji bora kutokana na idadi ya michezo iliyosalia, wanatakiwa kuendelea kukaza buti,” aliongeza Msuva.

Kwa sasa Msuva anaendelea na programu binafsi akisubiri muafaka wa kesi yake na Wydad iliyoko FIFA.

SIMBA WAIFANYIA UMAFIA ASEC…MO DEWJI ATUA KAMBINI…RAIS SAMIA AHUSISHWA KWENYE MCHAKATO… WAKATI SIMBA IKIZIDI KUVUNJA REKODI ZA AL AHLY CAF…BARBARA KUMBE ALISHALIONA HILO MAPEMA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply