Azam FC

BAADA YA KUFUNGA GOLI LAKE LA KWANZA MSIMU HUU..DUBE AMCHIMBA MKWARA MAYELE…

admin March 21, 2022 5:36 pm


STRAIKA wa Azam FC, Prince Dube, amesema kwa sasa anahitaji kufunga mfululizo ili kuisaidia timu yake kumaliza ligi kwenye nafasi nzuri na kuwania Tuzo ya Ufungaji Bora msimu huu.

Dube aliyasema hayo baada ya kufanikiwa kufunga bao lake la kwanza msimu huu wakati Azam FC ikiibuka na ushindi wa mabao 1-2 dhidi ya Namungo kwenye Uwanja wa Ilulu, Lindi.

Wakati Dube akiwa na bao moja, kinara wa mabao Ligi Kuu Bara msimu huu ni Fiston Mayele wa Yanga mwenye kumi kabla ya mchezo wa jana sawa na Reliants Lusajo wa Namungo.

Dube, alisema: “Namshukuru Mungu kwa kufunga bao langu la kwanza msimu huu, nafikiri huu ndiyo mwanzo wa safari yangu ya kufunga mfululizo ili kuisaidia timu yangu.

“Najua wengi wanataka kujua kama naweza kuwania Tuzo ya Ufungaji Bora, ngumu kusema kwa sababu watu wapo mbali, ingawa kila kitu kinawezekana kwa juhudi na maombi.”

KASI YA YANGA KWENYE LIGI YAWATISHA SIMBA…WAITANA KWA SIRI SIRI KUIJADILI…ISHU NZIMA IKO HIVI… UKIMKABA OVYO MAYELE..JUA UMEKWISHA…RAGE AIBUKA NA JIPYA SIMBA…PABLO ALA KIAPO KIPYA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply