Home Habari za michezo RAGE ACHOCHEA KUNI ISHU YA UBINGWA KWA YANGA…ATUPA KOMBORA HILI SIMBA…

RAGE ACHOCHEA KUNI ISHU YA UBINGWA KWA YANGA…ATUPA KOMBORA HILI SIMBA…


ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, ameitaka timu hiyo kufanya kazi ya ziada kama kweli wanataka kuishusha Yanga kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Rage alifunguka kuwa, Simba wapo kwenye nafasi kubwa ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, ila haitakuwa rahisi kwa sababu Yanga ya msimu huu ipo imara zaidi ya misimu mingine ya nyuma.

Akizungumza na Spoti Xtra Rage aliweka wazi kuwa: โ€œNaomba niwe muwazi juu ya suala hili, Yanga wapo imara sana msimu huu. Hivyo Simba wanatakiwa kuwa makini nao sana na wanatakiwa kufanya kazi kweli.

โ€œUbingwa unaweza kupatikana lakini siyo rahisi kama ambavyo ilikuwa misimu iliyopita, hilo wanatakiwa walijue, wana kazi kubwa ya kufanya”

SOMA NA HII  KWANGUA MPUNGA LEO HII NA MECHI ZA EUROPA...