Tetesi za Usajili Simba
Habari za michezo

SAMATTA AWATAMBIA WA NIGER KUWANIA TIKETI YA KOMBE LA DUNIA

Staff Desk November 17, 2023 11:16 am

Nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars wameweka wazi kuwa watapambana kupata matokeo kwenye mchezo wao dhidi ya Niger ambao ni wa kufuzu Kombe la Dunia. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Novemba 18 katika Mji wa Marrakech siku ya Jumamosi.

Miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye msafara huo ni Simon Msuva, Novatus Dismas, Peter Banda, Aishi Manula, Dickson Job, Mbwana Samatta.

Nahodha Samatta amesema kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu na ushindani mkubwa watakwenda kupambana kupata matokeo chanya.

Simon Msuva ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya kupambania taifa kwenye mechi zote za ushindani.

“Tupo hapa kwa ajili ya kupambania taifa a tunajua kuna ushindani mkubwa lakini tupo tayari na tutafanya vizuri,”.

UONGOZI WA YANGA KUNUNUA KILA GOLI LAKI 5 HAPA SIMBA WAVUNJE TU BENKI MAANA SIO KWA DAU HILI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply