Habari za michezo

RAGE ACHOCHEA KUNI ISHU YA UBINGWA KWA YANGA…ATUPA KOMBORA HILI SIMBA…

admin March 22, 2022 6:46 am


ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, ameitaka timu hiyo kufanya kazi ya ziada kama kweli wanataka kuishusha Yanga kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Rage alifunguka kuwa, Simba wapo kwenye nafasi kubwa ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, ila haitakuwa rahisi kwa sababu Yanga ya msimu huu ipo imara zaidi ya misimu mingine ya nyuma.

Akizungumza na Spoti Xtra Rage aliweka wazi kuwa: “Naomba niwe muwazi juu ya suala hili, Yanga wapo imara sana msimu huu. Hivyo Simba wanatakiwa kuwa makini nao sana na wanatakiwa kufanya kazi kweli.

“Ubingwa unaweza kupatikana lakini siyo rahisi kama ambavyo ilikuwa misimu iliyopita, hilo wanatakiwa walijue, wana kazi kubwa ya kufanya”

BAADA YA KUONA MAMBO YANAZIDI KUWA MAGUMU…KOCHA SIMBA AKUBALI YAISHE..AWAPA UBINGWA YANGA… BAADA YA KUONA YANGA WANAZIDI KUSHINDA…AHMED ALLY ASHINDWA KUJIZUIA…AWATOLEA POVU HILI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply