Home Habari za michezo KANOUTE AWAGOMEA MABOSI SIMBA…NI KUHUSU ISHU YA KUSEPA…ISHU NZIMA IKO HIVI…

KANOUTE AWAGOMEA MABOSI SIMBA…NI KUHUSU ISHU YA KUSEPA…ISHU NZIMA IKO HIVI…


WACHEZAJI wa Simba waliokuwa hawana majukumu ya timu za taifa walipewa mapumziko ya siku tano na baadhi waliamua kutimkia makwao, lakini kiungo Sadio Kanoute aligoma kabisa kuondoka.

Kanoute alishuhudiwa akiwa bize na mazoezi ya gym eneo la Mbezi na alipoulizwa alisema mechi ya mwisho dhidi ya Asec Mimosas hakucheza kutokana na maumivu ya mguu aliyokuwa akiyasikia na hata kushindwa kufanya mazoezi ya mwisho siku moja kabla ya mchezo wakiwa Benin.

Alisema walipewa ruhusa alikuwa na nafasi ya kwenda kwao Mali kusalimia familia kwa siku chache ili Machi 27, awepo kambini kuungana na wenzake kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa mwisho hatua ya makundi kombe la Shirikisho Afrika.

“Wala sikutaka kwenda nyumbani ila nimeamua katika kipindi hichi cha mapumziko kufanya mazoezi yangu binafsi mengi zaidi kama hivi ambavyo umenikuta hapa,” alisema Kanoute na kuongeza;

“Nimeamua kufanya hivi kurudisha utimamu wangu wa mwili niliokuwa nao kabla ya kushindwa kucheza mechi iliyopita kwani yale maumivu yalikuwa yakinisumbua sasa hivi hayapo tena na baada ya kurejea kambini kuungana na wachezaji wenzangu naimani nitakuwa fiti.”

SOMA NA HII  UBAYA UBWELA WAZUA BALAA KWA WAPINZANI