Habar za Usajili Simba

DUH…WAWA NDIO BASI TENA SIMBA…’MAJEMBE MAPYA YA MAANA KUTUA’..SABABU HIZI HAPA…

admin March 29, 2022 6:32 am


Ni suala la muda tu. Mwisho wa msimu huu Simba itasajili wachezaji wanne wa kigeni ili kuongeza makali ya kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao.

Ili Simba ishushe majembe hayo akiwamo Victorien Adebayor wa USGN ya Niger ni lazima iwaache wengine ipatikane nafsi ya wapya kuingia, huku moja ya jina linalotajwa litakalokuwa la kwanza ni Pascal Wawa.

Kanuni ya usajili inaruhusu klabu kusajili wachezaji 12 wa kigeni na kwa sasa Simba imeshajaza, lakini mabosi wao wameanza kumalizana na nyota wapya ili watue Msimbazi na Wawa anahesabiwa siku.

Wawa ilikuwa aachwe mwishoni mwa msimu uliopita, ila kocha wa Simba, Didier Gomes aliwapa masharti magumu mabosi zake na suala la kumuacha beki huyo lilikwama.

Tangu aondoke kocha Didier Gomes, Wawa amekuwa na wakati mgumu kucheza mara kwa mara kama ilivyokuwa misimu miwili iliyopita na pia mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu sambamba na nyota wengine 12.

Katika nafasi ya beki wa kati anayocheza, Joash Onyango na Henock Inonga wanacheza mara kwa mara. Miongoni mwa sababu zinazotajwa Wawa kuachwa ni kushindwa kucheza kikosi cha kwanza, umri mkubwa, kufanya makosa ya kiulinzi mara kwa mara, kutocheza kwa ubora kama wakati aliotua hapa nchini.

Kuondoka kwake kutafungua mlango beki wa kigeni kutua Msimbazi.

FEI TOTO AONGEZA IDADI YA WAGONJWA KWENYE ‘WODI YA YANGA’…ATEMWA TAIFA STARS JUMLA JUMLA.. MANARA ‘APIGILIA NYUNDO’ ISHU YA MAYELE KUTAKIWA KAIZER CHIEF…ATUPA DONGO SIMBA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply