BENCHI la Ufundi la Simba chini ya Kocha Mkuu, Pablo Franco, lina matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika mchezo wa mwisho wa Kundi D katika Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Gendarmerie. Hiyo ni baada ya kufanya marekebisho ya makosa ya mchezo uliopita dhidi ya ASEC Mimosas ambapo Simba ikiwa ugenini, ilifungwa 3-0.
Jumapili ya wiki hii, Simba itaikaribisha Gendarmerie kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, ambapo inahitaji ushindi ili kufuzu robo fainali. Kocha Msadizi wa Simba, Selemani Matola, alisema mchezo dhidi Gendarmerie lazima wapate ushindi ili wafuzu robo fainali.
Matola alisema wameona upungufu kupitia michezo iliyopita, hivyo mara baada ya juzi kuingia kambini, wameanza kuyafanyia kazi kuhakikisha wanapata ushindi. Aliongeza kuwa, kati ya nafasi ambayo inahitaji marekebisho ni safu ya ushambuliaji kwani wanatengeneza nafasi nyingi, lakini wanashindwa kuzitumia vema kufunga mabao.
“Tumeingia kambini leo (juzi) tukiwa tunafahamu umuhimu mkubwa wa mchezo dhidi ya Gendarmerie ambao kwetu ni muhimu kushinda ili tufuzu robo fainali. “Katika michezo iliyopita ambayo tumefungwa dhidi ya ASEC na RS Berkane, kuna baadhi ya makosa ambayo wachezaji wetu waliyafanya ambayo tumepanga kuyafanyia kazi baada ya kuingia kambini. “Hivyo hatutaki kuona yakitokea tena katika mchezo huu kwa sababu tunahitaji kufi kia malengo ya kuifi kisha timu robo fainali,” alisema Matola.