Home Habari za michezo AHMED ALLY – KUPONA KWA MKUDE ILIKUWA NI BAHATI MBAYA KWA WAARABU…ALIWAFANYA...

AHMED ALLY – KUPONA KWA MKUDE ILIKUWA NI BAHATI MBAYA KWA WAARABU…ALIWAFANYA VIBAYA SANA..


BAADA ya kupata pointi tatu za nyumbani, uongozi wa Simba umeibuka na kumtaja kiungo wao mkabaji Jonas Mkude ndiye aliyekuwa kikwazo kwa wapinzani wao RS Berkane ya nchini Morocco.

Simba ilifanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Berkane katika mchezo wa nne wa Kundi D, uliopigwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa.

Bao la Simba lilifungwa na Msenegali, Pape Ousmane Sakho baada ya kuwachambua mabeki wa Berkane kabla ya kupiga shuti ndani ya 18 na kujaa wavuni.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema kuwa moja ya bahati mbaya waliyokutana nayo Berkane ni kupona na kurejea kwa Mkude aliyemiliki vizuri safu ya kiungo kwa dakika zote 90.

Ally alisema kuwa katika mchezo uliopita waliocheza Morocco alikosekana Mkude ambaye yeye walikuwa hawamjui na kutegemea kuwepo kiungo wa aina yake mwenye uwezo wa kukaba na kuchezesha timu ndani ya wakati mmoja.

“Berkane kule kwao walidhani maisha ni rahisi kwa sababu moja ya nguzo muhimu ya Simba ambaye ni Mkude haikuwepo baada ya kuugua ghafla tukiwa Niger tulipokwenda kucheza dhidi ya Gendarmerie kabla ya kuelekea Morocco.

“Hivyo Mkude aliwafanya vibaya na kuwavuruga vibaya katikati safu ya kiungo, na hiyo ni kutokana kutomuona katika mchezo wa kwanza tuliocheza nyumbani kwao Morocco.

“Hiyo ni moja ya silaha zetu tulizozificha kwa Berkane, wenyewe walijua kuwa kikosi chetu ndiyo kimefikia mwisho baada ya baadhi kutowaona akiwemo huyo Mkude,” alisema Ally.

SOMA NA HII  BAADA YA YANGA KUFUNGWA JANA....ALLY KAMWE KAIBUKA NA HILI JIPYA LA KUTULIZIA HALI....