Home news BAADA YA SIMBA KUTUA TZ…PABLO ATEMA NYONGO…APIGA MARUFUKU WACHEZAJI KWENDA KULALA…

BAADA YA SIMBA KUTUA TZ…PABLO ATEMA NYONGO…APIGA MARUFUKU WACHEZAJI KWENDA KULALA…


Kocha Mkuu wa Simba SC Franco Pablo Martin amesema wachezaji wake hawatakua na muda wa kupumzika baada ya kuwasili Dar es salaam, wakitokea nchini Morocco.

Simba SC imewasili leo Jijini humo, baada ya majuma mawili ambayo yalishuhudia wakipambana ugenini kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya USGN ya Niger na RS Berkane ya Morocco.

Kocha Pablo amesema wachezaji wake watalazimika kuanza maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Biashara United Mara moja kwa moja, kutokana na Ratiba ya ligi hiyo kuwabana.

Amesema alitamani wachezaji wake wangepata muda wa kupumzika lakini hana budi kuendelea na kazi ya kuwandaa kwa mchezo huo, ambao utapigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Ijumaa (Machi 04).

“Wachezaji hawatapata muda wa kupumzika, moja kwa moja tutaanza maandalizo ya mchezo wetu wa Ligi Kuu ambao unatukabili baada ya kumaliza shughuli ya kupambana ugenini kimataifa.”

“Ingependeza kama wachezaji wangepata muda wa kupumzika, lakini sina namna nyingine zaidi ya kuendelea na kazi ya kuhakikisha tunacheza mchezo wetu wa Ligi Kuu na kupata matokeo mazuri.” Amesema Kocha huyo kutoka nchini Hispania.

Simba SC ilipoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya RS Berkani Jumapili (Februari 27), huku ikiambulia sare ya 1-1 dhidi ya USGN ugenini (Februari 21).

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI DHIDI YA SIMBA...MAYELE AFUNGUKA ATAKAVYOWATETEMESHA KINA ONYANGO....