Home news MASAU BWIRE APATA AJALI…AFUNGUKA ALIVYOGONGWA…AISIFU GARI YAKE KUWA NGUMU…

MASAU BWIRE APATA AJALI…AFUNGUKA ALIVYOGONGWA…AISIFU GARI YAKE KUWA NGUMU…


MSEMAJI wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amepata ajali maeneo ya Buguruni jijini Dar es Salaam leo Machi 3 mchana akiwa na gari yake aina ya Toyota Rav 4.

Akizungumza na gazeti la Mwanaspoti, Bwire amesema, ajali hiyo imetokea mchana huu akiwa njiani kuelekea Mzizima.

”Nilikuwa natokea Ilala Boma nafika Buguruni nakutana na shida hiyo kusema ukweli huyo jamaa amenigonga, ila niko salama,” anasema Bwire.

“Daladala imetaka kunipita basi nikamtizama kwenye kioo akaja akanivaa, sema gari ni ngumu ingekuwa gari nyepesi ingeharibika sana,”

Anasema kwa mbele na nyuma ya gari yake ndipo palipopata shida sana.

SOMA NA HII  BAADA YA MATOLA KUSEPA ...MGUNDA ASHUSHA KITU KINGINE SIMBA...MABOSI WAMPITISHA CHAP HARAKA...