Home news NABI KWELI NI ‘BABA LAO’ …AWATIMULIA VUMBI WENZAKE KWA UBORA…KOCHA WA SIMBA...

NABI KWELI NI ‘BABA LAO’ …AWATIMULIA VUMBI WENZAKE KWA UBORA…KOCHA WA SIMBA CHALII….


Nasreddine Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga ameteuliwa kuwa kocha bora wa Februari ndani ya Ligi Kuu Bara.

Kwa mujibu wa Kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Soka Tanzania,  (TFF) iliyokutana Jumamosi ilimchagua  Nabi.

Nabi ametwaa tuzo hiyo akiwashinda Fred Minziro wa Geita Gold na Thiery Hitimana wa KMC ambaye awali alikuwa kocha msaidizi wa Simba SC.

Kwa Februari Yanga iliifunga Kagera Sugar mabao 3-0, Mtibwa Sugar 0-2 Yanga na sare ya bila kufungana dhidi ya Mbeya City.

Leo Yanga imeibuka na ushindi mbele ya Geita Gold, mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

SOMA NA HII  YANGA SC YATOA WAWILI KIKOSI BORA SHIRIKISHO