Home news TIMU YA TAIFA U-17 YATOA KICHAPO CHA KUFA MTU HUKO….WAJIWEKA ‘MBELEMBELE’...

TIMU YA TAIFA U-17 YATOA KICHAPO CHA KUFA MTU HUKO….WAJIWEKA ‘MBELEMBELE’ KUFUZI KOMBE LA DUNIA…


TIMU ya taifa ya Tanzania, U 17 ya Wanawake imeshinda mabao 7-0 dhidi ya Botswana kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Amaan,Zanzibar.

Ni mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia ambao ulikuwa na ushindani mkubwa.

Kipindi cha kwanza Tanzania ilikuwa mbele kwa mabao manne na kipindi cha pili walifunga mabao  matatu na kufanya hesabu kukamilika kwa kifurushi cha mabao 7-0.

Watupiaji walikuwa ni Neema Paul ambaye alifunga mabao mawili, Clara Luvanga yeye alitupia mabao mawili na nyota Aisha Juma yeye alitupia mabao matatu.

SOMA NA HII  MERIDIANBET KASINO INAKULETEA MCHEZO WA MAOKOTO COBRA QUEEN.