Home Uncategorized SAKATA LA MKWANJA KUMPONZA RAIS WA CAF LAWAIBUA TFF

SAKATA LA MKWANJA KUMPONZA RAIS WA CAF LAWAIBUA TFF


SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa ufafanuzi juu ya kuhusishwa kwa Rais wake, Wallace Karia, katika malipo yanayodaiwa kusababisha Shirikisho la Mpira wa Miguu (FIFA) kumfungia miaka mitano Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Ahmad Ahmad.


Jana taarifa ilitolewa kuwa Ahmad amefungiwa miaka mitano kutokana na matumizi mabaya ya fedha baada ya kufanyiwa uchunguzi kwa muda mrefu.

Kamati ya maadili imesema kuwa kiongozi huyo alitoa na kupokea rushwa pamoja na matumizi mabaya ya ofisi jambo ambalo limemuweka kando kwenye masuala ya uongozi.


Mbali na adhabu hiyo anatakiwa kulipa randi milioni 3.3, taarifa kutoka TFF imeeleza kuwa tetesi ambazo zimekuwa zikimuhusisha Rais Wallace Karia hazina ukweli kwa kuwa hakuna fedha za Caf ambazo zimewahi kuingia kwenye akaunti binafsi ya Karia.

Taarifa imefanunua namna hii:-


SOMA NA HII  MECHI YA SIMBA NA MTIBWA YAPANGULIWA, RATIBA MPYA YATAJWA