Home news PAMOJA NA ‘KUTOBOLEWA TUNDU MOJA’ NA YANGA…GEITA GOLD WAOGA MISIFA KEMKEM..

PAMOJA NA ‘KUTOBOLEWA TUNDU MOJA’ NA YANGA…GEITA GOLD WAOGA MISIFA KEMKEM..


Licha ya kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Young Africans katika mchezo wa Mzunguuko wa 17 wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Wachezaji wa Geita Gold FC wamepongezwa na Uongozi wa klabu hiyo.

Geita Gold FC ilipoteza mchezo huo Jumapili (Machi 06) katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, baada ya kuuhamisha mchezo huo kutoka mkoani Geita kwenye Uwanja wa Nyankumbu.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Geita Gold FC Simon Shija amesema hawana budi kuwapongeza wachezaji wao kwa kazi kubwa waliyoifanya katika mchezo huo, licha ya kushindwa kuwika katika Uwanja wao wa nyumbani.

Shija amesema wachezjai wao kwa ujumla walionyesha kupambana hadi mwisho, na dhamira yao ilikua ni kuibuka na ushindi ambao ungewapa alama tatu, ila mambo yalikwenda tofauti.

“Katika mchezo kuna matokeo matatu Kupoteza, Kushinda na Kutoa Sare, sisi tumepoteza mchezo, haimaamini kupoteza kwetu ndio tukae kimya na tusiseme chochote, kwa hakika wachezaji wetu walionyesha kupambana na walidhamiria kushinda dhidi ya Young Africans ila bahati haikua kwao.”

“Ukiangalia Soka walilocheza lilikua na kila sababu ya kuona Geita ni timu ya aina gani, hivyo sisi kama viongozi hatuna budi kutoa pongezi kwa wachezaji wetu.” Amesema Shija.

Bao pekee la Young Africans katika mchezo huo lilipachikwa wavuni na Mshambuliaji wao kutoka DR Congo Fiston Kalala Mayele katika Dakika ya kwanza ya mchezo.

Ushindi huo unaendelea kuifanya Young Africans kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 45, ikifuatiwa na Bingwa Mtetezi Simba SC yenye alama 37.

Geita Gold ipo nafasi ya 08 ikiwa na alama 21, baada ya kushuka dimbani mara 17.

SOMA NA HII  KISA UBINGWA...ALLY KAMWE ATAKA MASHABIKI YANGA WASIMSIKILIZE MANARA.....