Home news WAKATI YANGA WAKIMUIMBA AUCHO KWA KIWANGO CHAKE…KOCHA MGANDA AWASHANGAA…ADAI ANAKIWANGO KIBOVU…

WAKATI YANGA WAKIMUIMBA AUCHO KWA KIWANGO CHAKE…KOCHA MGANDA AWASHANGAA…ADAI ANAKIWANGO KIBOVU…


KAMA unadhani kiungo wa Yanga, Khalid Aucho yupo kwenye kiwango kikubwa basi unajidanganya kwani mchezaji huyo ameshuka katika asilimia alizokuwa nazo wakati anaichezea timu ya Taifa Uganda ‘The Cranes’ kwenye fainali ya Mataifa Afrika (AFCON) 2019 nchini Misri.

Aliyekuwa kocha msaidizi wa timu hiyo na sasa ni kocha mkuu wa Mbeya City, Mathias Lule amefichua siri ya mchezaji huyo licha ya kufanya vizuri akiwa na Yanga bado hajarudi kwenye kiwango alichokuwa nacho AFCON.

Lule alisema siku zote Aucho ni mchezaji mzuri na bora kwenye timu lakini kwa sasa licha ya kufanya vizuri ndani ya Yanga anamwona anacheza chini ya kiwango.

“Aucho yule wa Afcon na huyu ni vitu viwili tofauti, inawezekana na maandalizi makubwa ambayo tulikuwa tumeyafanya tukijiandaa na fainali hizo ndio maana alikuwa bora,” alisema kuongeza;

“Wakati ule alikuwa na asilimia 90 hivyo alitupa vitu vyote ndani ya uwanja, huyu wa Yanga bado yupo kwenye asilimia 60-70 na ikitokea akafika asilimia zile za nyuma atawapa kitu kikubwa zaidi ya sasa, siwezi kusema kitu sana labda kwa nini amekuwa hivi kwa sababu sipo naye kwa sasa.”

Lule alisema bado ana nafasi ya kufanya makubwa na kupandisha asilimia zake kwa sababu mchezaji huyo bado umri wake ni mdogo hivyo muda anao wa kujiweka sehemu nzuri.

Aucho amesajiliwa msimu huu akiwa mchezaji huru na tangu alipoingia katika timu hiyo amejihakikishia nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza.

SOMA NA HII  SIKU KADHAA KABLA YA KUKIPIGA NA AL AHLY...BENCHIKHA KAJA NA 'PIGO' HILI MATATA....