Home news BAADA YA KUONA YANGA WAMEWAZIDI KWA POINT 11…TRY AGAIN KAKUNA KICHWA WEE..KISHA...

BAADA YA KUONA YANGA WAMEWAZIDI KWA POINT 11…TRY AGAIN KAKUNA KICHWA WEE..KISHA AKASEMAA HAYA…


LICHA ya Yanga kutambia pointi 11 zaidi ilizoipiku Simba katika harakati za ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ ameonya wana mechi 15 watakazocheza kimkakati na wanaamini kushangaza wengi.

Amesisitiza; “Sawa tunaanza mzunguko wa pili tukiwa tumezidiwa pointi 11, lakini tuna mechi 15 mbeleni, hivyo tusubiri, msiwe na haraka na mambo.”

Yanga Jumapili iliyopita ilifikisha pointi 42 na kujiimarisha kileleni kwenye msimamo ikiwapiku watani zao Simba kwa pointi 11 na kesho Wekundu wa Msimbazi wataikaribisha Biashara United ikiwa ni mechi yao ya kwanza ya mzunguko wa pili.

Hadi sasa Simba ni ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 31 na ikishinda itafikisha 34 na kupunguza gepu la pointi.

Tofauti ya pointi hizo zimesababisha baadhi ya wapenzi wa Yanga kutamba kasi hiyo haitoshuka kwenye mzunguko wa pili na kila timu ishinde mechi zake.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema “Pointi 11 hadi watufikie maana yake washinde mechi tatu na kutoka sare michezo miwili, wakati huo sisi tunafungwa, jambo ambalo wasilitarajie, Yanga hii ni moto mwingine.”

Jana Try Again alisema “Timu imerejea na tunaelekeza nguvu kwenye ligi kuendeleza safari yetu ya kutetea ubingwa, hii ni ligi sio mtoano, hivyo yeyote anaweza kufungwa na kushinda na kibao kikageuka wakati wowote.

“Sawa tunaanza mzunguko wa pili tukiwa tumezidiwa pointi 11, lakini tuna mechi 15 mbeleni, hivyo tusubiri kuona bingwa atakuwa ni nani mwishoni mwa msimu.”

Alisema msimu uliopita pia waliingia kwenye mechi za mzunguko wa pili wakiwa wameachwa kwenye msimamo, lakini kibao kiligeuka na kutwaa ubingwa.

WAPINDUA MEZA

Ukichana na kichapo ilichopata Simba cha mabao 2-0, dhidi ya RS Berkane katika mchezo wa hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika ila mwenendo mzima wa timu hiyo umeimarika tofauti na ilivyoanza msimu.

Tangu ifungwe bao 1-0, kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar Januari 26, mwaka huu timu hiyo imekuwa na matokeo mazuri kuanzia makombe ya ndani hadi yale ya kimataifa ikicheza michezo saba kati yake ikishinda mitano, sare moja na kupoteza mmoja.

Ilianza kutoa kichapo kizito cha mabao 6-0, dhidi ya Dar City Januari 30, 2022, mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) hatua ya 32, kisha ushindi wa bao 1-0, dhidi ya Tanzania Prisons Februari 3 na Mbeya Kwanza Februari 6.

Baada ya hapo ikaanza kampeni ya hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika Februari 13, kwenye Uwanja wa Mkapa na iliendeleza moto wake kwa kushinda mabao 3-1, dhidi ya Ases Mimosas kutoka Ivory Coast, kabla ya kuishushia kipigo wazee wa ‘kupapasa’ Ruvu Shooting cha mabao 7-0, katika mchezo wa ASFC hatua ya 16 bora uliochezwa Februari 16, Uwanja wa Mkapa.

SOMA NA HII  ETIENNE NDAYIRAGIJE ALA SHAVU BURUNDI

Michezo miwili iliyofuata ni ya Kombe la Shirikisho Afrika ikitoka sare ya kufungana bao 1-1, dhidi ya Gendarmerie Nationale ya Niger katika mchezo wa pili wa hatua ya makundi Februari 20, kabla ya kufungwa 2-0, na RS Berkane ya Morocco.

Licha ya kupoteza mchezo huo ila bado Simba iko kwenye wakati mzuri wa kufuzu hatua ya makundi ya Kombe hilo kwani iko nafasi ya pili na pointi nne, ikihitaji pointi sita tu ili kujihakikishia nafasi hiyo kutokana na kusaliwa na michezo miwili ya nyumbani dhidi ya RS Berkane Machi 13, na Gendarmerie Nationale April 3, Uwanja wa Mkapa na mmoja wa ugenini dhidi ya Asec Mimosas Machi 20.

Kabla ya kuanza hesabu za michezo hiyo itakayoamua hatima yao, ila wanakabiliwa na pengo la pointi 11 kwenye Ligi Kuu Bara kutoka kwa wapinzani wao Yanga waliojikusanyia pointi 42, katika michezo 16, huku Simba ikiwa na pointi 31, baada ya michezo 15.

Kesho itakuwa kwenye Uwanja wa Mkapa kucheza na Biashara United na katika mchezo wao wa raundi ya kwanza waliokutana katika Uwanja wa Karume Musoma Septemba 28, 2021, zilitoka suluhu ya 0-0, huku nahodha wa Simba John Bocco akishindwa kuipatia timu yake pointi tatu muhimu baada ya kukosa mkwaju wa penalti iliyodakwa na kipa James Ssetupa dakika ya mwisho ya mchezo.

Nyota wa zamani wa timu hiyo, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ alisema Simba bado ni imara tofauti na wengi wanavyoichukulia kwa sababu wachezaji wengi ni bora ila kinachowagharimu ni uchovu wa wachezaji wao muhimu kutokana na kucheza kwa misimu minne mfululizo.

“Bado wana nafasi kubwa ya kurejea katika ubora wao, unajua sio rahisi wachezaji wale wale kutumika kwa muda mrefu ingawa kwa jinsi wanavyozidi kupata matokeo chanya, inawaongezea morali kubwa na hali ya kujiamini zaidi.” alisema.

Naye Kocha wa zamani wa KMC na Mkufunzi wa makocha nchini, John Simkoko alisema.

“Endapo watatulia na kuacha kucheza kwa presha ya kuwaangalia wengine, naamini kabisa bado wana timu shindani na imara inayoweza kuleta athari kwa wapinzani wao wengine.”