Home Uncategorized MTAMBO WA MABAO KAGERA SUGAR WAFUNGUKIA USAJILI WAKE YANGA

MTAMBO WA MABAO KAGERA SUGAR WAFUNGUKIA USAJILI WAKE YANGA


 YUSUPH Mhilu mshambuiaji namba moja ndani ya kikosi cha Kagera Sugar amesema kuwa kwa sasa yeye ni mali ya Kagera Sugar hivyo atapambana kufikia malengo ya timu hiyo kwa msimu wa 2020/21.

Nyota huyo ambaye alikuwa anatajwa kuibukia Yanga ameweka wazi kwamba bado haijawa rasmi kuhusu dili hilo hivyo anafikiria maisha yake ndani ya kikosi hicho.

Msimu huu alianza kwa kusuasua ambapo alikuwa nje kutokana na kile alichoweka wazi kwamba ni kusumbuliwa na majeraha ya nyama za misuli aliporejea uwanjani alianza kwa kucheka na nyavu.

Mchezo wake wa kwanza alifunga bao la ushindi wakati Kagera Sugar ikishinda bao 1-0 dhidi ya KMC ambayo ilikuwa kwenye ubora wake Uwanja wa Kaitaba, Kagera.


Akizungumza na Saleh Jembe, Mhilu amesema kuwa bado timu hiyo ina nafasi ya kufanya vizuri ndani ya Ligi Kuu Bara.

“Bado mimi ni mchezaji wa Kagera Sugar ishu yangu ya kuondoka ninaskia ila bado nipo kwa hapa wakati huu kikubwa ni kuzidi kupambana timu ipate matokeo.

“Kuondoka inawezekana ila mpaka pale utaratibu utakapofuatwa kwani masuala ya mchezaji kupata changamto mpya ipo kila mahali,” .

Kagera Sugar ikiwa imefunga mabao 18 amehusika kwenye mabao manne ambayo aliyatupia yeye mwenyewe.

SOMA NA HII  MPOKI ALIVYOMVUNJA MBAVU MO DEWJI - VIDEO