Home Uncategorized JESHI LA AZAM FC LAKWEA PIPA KUIFUATA MWADUI FC

JESHI LA AZAM FC LAKWEA PIPA KUIFUATA MWADUI FC


TIMU ya Azam FC iliyo chini ya Arstica Cioaba, leo imekwea pipa kuelekea mkoani Shinyanga kwa ajili ya mchezo wao wa ligi dhidi ya Mwadui FC.

Mchezo huo utachezwa kesho, Januari,22 Uwanja wa Kambarage. Kikosi cha Azam FC kimetumia usafiri wa ndege wa Shirika la ndege Tanzania, AirTanzania.

Cioaba amesema kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu ila watapambana kutafuta pointi tatu muhimu.

Azam FC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa imecheza mechi 15 na ina pointi 32.

SOMA NA HII  MSUVA AIPA AHUENI STARS BURUNDI, MECHI YAMALIZIKA 1-1

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here