Home Uncategorized MANCHESTER UNITED WAMEAMUA KUINASA SAINI YA KINDA HUYU

MANCHESTER UNITED WAMEAMUA KUINASA SAINI YA KINDA HUYU

MANCHESTER United imeingia kwenye vita ya kuwania saini ya kinda anayekipiga ndani ya Klabu ya Birmingham City mwenye uwezo mkubwa Jude Bellingham.

Ripoti zinaeleza kuwa nyota huyo alionana na kocha wa zamani wa United Alex Ferguson ambaye alizungumza naye kuhusus suala la kumhamisha kwenye klabu yake anayocheza kwa sasa ambapo alipata muda wa kuzungumza na familia yake pia.
Kinda huyo mwenye miaka 16 anapigiwa hesabu pia na klabu mbili kubwa ikiwa ni pamoja na Borussia Dortmund na Chelsea ambazo zimeonyesha nia ya kupata saini yake.
United inapewa nafasi kubwa ya kupata saini ya kinda huyo ambapo inaelezwa kuwa wametenga dau la pauni milioni 50 ambapo awali walikuwa wameandaa dau la pauni milioni 35 kutokana na ushindani wameamua kupandisha dau ili kuipata saini ya kinda huyo.
SOMA NA HII  VPL:YANGA 1-1 DODOMA JIJI