Home Uncategorized PAMBA FC WAMEFUNGUA NJIA WENGINE TUFUATE, KATIKA HILI PONGEZI MNASTAHILI

PAMBA FC WAMEFUNGUA NJIA WENGINE TUFUATE, KATIKA HILI PONGEZI MNASTAHILI


WAKATI huu wa janga la maambukizi ya Virusi vya Corona timu nyingi zimeanza kuonyesha vita kwa vitendo jambo ambalo linahitaji pongezi na kuungwa mkono pia.

Kwenye ulimwengu wa soka kwa sasa bado ganzi inaendelea ambapo wanamichezo wengi wanashinda nyumbani kulinda vipaji vyao.

Hii inatokana na kusimamishwa kwa Ligi nyingi duniani jambo lililofanya shughuli za michezo na kusimama pia.

Klabu ya Pamba SC hivi karibuni leo ilitembelea kituo cha Watoto Yatima kwa ajili ya kuwajulia hali pamoja na kuwapa misaada kwa kile ambacho walijaliwa.

 Kituo cha watoto wenye uhitaji maalumu cha kulea na kuwasaidia Watoto waliofanyiwa ukatili Cha Foundation karibu Tanzania kilichopo Kiloleli Jijini Mwanza kilipata faida kubwa ya kuongeza familia na marafiki wapya achilia mbali kufarijika pamoja.

 Pia wana Pamba walipeleka baadhi ya Vifaa ikiwa ni pamoja  na kugawa vitakasa mikono ikiwa ni Sanitizer kwa kila mtoto pamoja na mahitaji mengine maalumu.

Hongereni Pamba kwa moyo huo Mungu awabariki na wengine pia ni muhimu kuungana kwenye vita hii kubwa kwani janga ni letu sote.

SOMA NA HII  HUU HAPA MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA BARA