Home Uncategorized UHONDO WA PREMIER KUREJEA JUNI 8

UHONDO WA PREMIER KUREJEA JUNI 8

IMEELEZWA kuwa, Ligi Kuu ya England maarufu Premier, huenda ikarejea wiki ya kuanzia Juni 8, mwaka huu baada ya kikao cha majadiliano ya lini wachezaji wataruhusiwa kufanya mazoezi ya pamoja kufanyika jana.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni baada ya ligi hiyo na ligi zingine duniani kusimama kutokana na janga la Corona ambali linaisumbua dunia kwa sasa.


Katika kikosi hicho, klabu zimekubaliana kuanza mazoezi  Mei 18, mwaka huu na mechi zitachezwa kuanzia Juni 8, huku Serikali ya Uingereza ikisema itahakikisha wachezaji wanafuata njia za kujilinda zaidi na Virusi vya Corona.

Mpaka Premier inasimama, Liverpool ilikuwa inaongoza ikiwa na pointi 82 ambapo katika mechi tisa ilizosalia nazo, inahitaji pointi sita tu kuwa mabingwa.


Endapo Liverpool itakuwa bingwa msimu huu, basi itakuwa ni mara ya kwanza baada ya kupita takribani miaka 30.

SOMA NA HII  BALINYA APEWA DAWA YA KUIMALIZA SIMBA HARAKA