Home Uncategorized MBEYA CITY: TUPO KWENYE KIPINDI KIGUMU KWA SASA,TUTATOKA

MBEYA CITY: TUPO KWENYE KIPINDI KIGUMU KWA SASA,TUTATOKA

AMRI Said, Kocha Mkuu wa Mbeya City amesema kuwa timu yake inapitia kipindi kigumu kwa sasa kutokana na kushindwa kupenya mbele ya KMC kwenye mchezo wao wa jana uliochezwa Uwanja wa Samora.

Mbeya City ilikubali kichapo cha bao 1-0 ikiwa nyumbani jambo lililowafanya wapoteza pointi zote tatu muhimu.

Said amesema:-“Tulijipanga kupata matokeo ila tulishindwa kuzitumia nafasi ambazo tulizipata na mpinzani wetu akatuzidi mbinu, ni matokeo mabaya kwetu tutapambana ili kurejea kwenye ubora,”.

Mbeya City ipo nafasi ya 18 ikiwa na pointi 14 huku KMC ikiwa nafasi ya 15 na pointi 20 zote zimecheza mechi 19.

SOMA NA HII  KUISHUHUDIA YANGA vs MADEAMA KIINGILIO NI MIGUU YAKO GSM AFANYA KWELI