Home Uncategorized KOCHA YANGA AGEUKA MBOGO KWA WACHEZAJI

KOCHA YANGA AGEUKA MBOGO KWA WACHEZAJI


Kocha wa Yanga, Luc Eymael amewacharukiwa wachezaji wa kikosi hicho baada ya kushindwa kutumia nafasi walizotengeneza kupata mabao ya haraka ambayo yangewatoa mchezoni wapinzani wao.

Eymael ametoa kauli hiyo baada ya kocha huyo kuanza vibaya kibarua chake kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Eymael alisema kikosi chake kipindi fulani walionekana kuzidiwa sehemu ya kiungo na wapinzani na kuwapa mwaya wa kufunga lakini walitengeneza nafasi nyingi kwenye eneo la hatari ambazo nyota wake walishindwa kutumia.

“Mchezo ulikuwa mgumu kwani wapinzani wetu walicheza kwa kujiamini na kumiliki sehemu ya kiungo pamoja na hivyo kwa kiasi fulani na tulikuwa wazuri kwa kutengeneza nafasi nyingi ambazo zilishindwa kutumika ipasavyo,” alisema Eymael.

Alisema kipindi cha pili wachezaji wake walionekana kurudia kufanya makosa yaliyowagharimu kipindi cha kwanza licha ya kupewa maelekezo na kujikuta wakiwaacha tena wapinzani kuchezea mpira kwa uhuru na kufunga tena mabao mawili.


SOMA NA HII  JKT TANZANIA YAICHAPA KAGERA SUGAR JAMHURI