Home Uncategorized MZUNGU WA SIMBA AMZUNGUMZIA MCHEZAJI WAKE AJIBU, HUU NDIO MTAZAMO WAKE

MZUNGU WA SIMBA AMZUNGUMZIA MCHEZAJI WAKE AJIBU, HUU NDIO MTAZAMO WAKE


SVEN Vanderbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kwa kiasi fulani ameanza kumuelewa mchezaji wake Ibrahim Ajibu.

Ajibu alijiunga na Simba akitokea Yanga ambapo akiwa huko msimu wa 2018/19 alikuwa kinara wa pasi za mwisho alitoa 17 na kufunga mabao sita kwa sasa akiwa ndani ya Simba ametoa pasi nne na kufunga bao moja.

Sven amesema kuwa Ajibu alibadilisha mchezo alipoingia wakati Simba ikishinda mabao 2-1 mbele ya Polisi Tanzania Uwanja wa Taifa.

“Kwa kiasi fulani kwenye mchezo wetu dhidi ya Polisi Tanzania alipoingia Ajibu, timu ilibadilika na kuanza kucheza mpira unaoeleweka na mipango kuwa imara mwisho wa siku tukashinda,” amesema.

Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa imecheza mechi 19 imejikusanyia jumla ya pointi 50 kibindoni.

SOMA NA HII  MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA BARA