Home news ALICHOKISEMA JAMHURI KIWHELO ‘JULIO’ KUHUSU KIWANGO CHA DICKSON JOB WA YANGA…

ALICHOKISEMA JAMHURI KIWHELO ‘JULIO’ KUHUSU KIWANGO CHA DICKSON JOB WA YANGA…


BEKI wa zamani wa Yanga na Toto African ya Mwanza, Ladislaus Mbogo kasema kiwango cha beki wa Yanga Dickson Job ni kizuri na akiendelea na spidi hiyo akijitunza atakuja kuwa mlinzi bora na msaada kwa taifa.

Akizungumza na Gazeti la  Mwanaspoti kuhusu mabeki bora wanaocheza nafasi ya ulinzi wa kati katika Ligi Kuu Bara, Mbogo alisema Job ni beki mzawa ambaye anakuja vizuri na atakuja kuwa na faida kwa nchi akiwa na mwendelezo huo.

Mbogo aliitumikia Yanga kwa mwaka mmoja kuanzia 2012 hadi 2013, lakini hakuwa na msimu mzuri kutokana na ushindani wa namba kwa kipindi hicho na kuuguza majeraha baada ya kufanyiwa upasuaji wa uvimbe kwenye shavu, ambapo kwa sasa anakipiga timu ya wakongwe ya Mwanza Veteran.

“Kwa Tanzania kuna mabeki wengi, ila ukimuona bwana mdogo kama Dickson Job ni beki ambaye unamuona akiendelea na mwenendo huo atakuwa na faida kwa nchi, kwa sababu anaitendekea haki nafasi yake. Anacheza vyema sana, anajua kunusa hatari na anaiokoa klabu yake. Kwa namna anavyocheza ananivutia na kunikumbusha enzi zangu,” alisema mchezaji huyo.

Mbogo aliwataja mabeki wengine ambao wanamvutia ni Yannick Bangala wa DR Congo anayekipiga Yanga na Kelvin Yondani anayecheza Polisi Tanzania, huku akionya Watanzania kutozingatia umri wa wachezaji na kuwahukumu, bali waangalie uwezo wao uwanjani.

“Kuna beki mmoja mgeni pale Yanga anaitwa Bangala kwa namna anavyocheza ananifurahisha sana, lakini bado hata wachezaji wa Kitanzania ukimwangalia mtu kama Kelvin Yondani japokuwa Watanzania tunakimbilia sana umri kuliko kuangalia uwezo wake, ila ni beki mzuri.”

Kauli ya Mbogo iliungwa mkono na Kocha Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’ ambaye alisema kiwango cha Job hakijaanzia Yanga tu, bali kilionekana tangu akiwa Mtibwa Sugar huku akimshauri kuendelea kupambana na Mungu atamsaidia.

“Dikson Job ana kipaji kikubwa cha kucheza mpira na ni kipaji ambacho kwa siku za mbeleni kitakuwa na manufaa kwa taifa zaidi, namuomba Mungu amsaidie yeye pia azidi kuongeza juhudi, kujituma na kuzidisha nidhamu bila kubweteka,” alisema Julio.

SOMA NA HII  OKWA WA IHEFU APANIA KUWAUMBUA SIMBA KWA KUMUACHA DIRISHA DOGO...ISHU YAKE IKO HIVI...