Home Uncategorized LIPULI YATAJA KILICHOWAKWAMISHWA KWA YANGA

LIPULI YATAJA KILICHOWAKWAMISHWA KWA YANGA

PAUL Nonga, nahodha na mshambuliaji wa Lipuli FC amesema kuwa walizidiwa mbinu kipindi cha kwanza na Yanga jana, Februari 5 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara jambo lililowafanya wakapoteza kwa kufungwa mabao 2-1.

Yanga ilipachika mabao yote mawili kipindi cha kwanza kupitia kwa Mapinduzi Balama na Bernard Morrison na lile la Lipuli lilipachikwa kipindi cha pili na David Mwasa kwa mpira wa adhabu uliojaa jumla kimiani.

Nonga amesema:-“Kipindi cha kwanza mbinu yetu ya kucheza ilifeli na kutufanya tushindwe kuzuia mashambulizi ya Yanga, ila mwisho wa siku ni matokeo tunayapokea tutajipanga kwa ajili ya mchezo wetu unaofuata,”.

Lipuli inashika nafasi ya 10 ikiwa na pointi 25 huku Yanga ikiwa nafasi ya tatu na pointi 34 kibindoni.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI