Home Uncategorized TIMU ZA MBEYA ZAMKAZIA MROMANIA WA AZAM FC

TIMU ZA MBEYA ZAMKAZIA MROMANIA WA AZAM FC


AZAM FC iliyo chini ya Arstica Cioaba raia wa Romania, imeshindwa kufurukuta mbele ya timu za Mbeya kwa kugawana pointi mojamoja kwenye mechi mbili za Ligi Kuu Bara.

Mchezo wa kwanza kwa timu ya Mbeya ilikuwa ni dhidi ya Mbeya City uliochezwa Uwanja wa Samora ambapo Azam FC ilikubali sare ya kufungana bao 1-1 na kugawana pointi moja.

Jana Uwanja wa Uhuru ililazimishwa sare na Prisons nayo ya Mbeya kwenye mchezo wa ligi baada ya kufungana bao 1-1.

Licha ya Azam FC kuanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa Obery Chirwa, Prisons walichomoa bao hilo dakika za usiku kupitia kwa Jumanne Elifadhili na kufanya ngoma iishe 1-1.

Azam FC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 38,Prisons ipo nafasi ya 11 na pointi zake 25 zote zimecheza mechi 19.

SOMA NA HII  KIFO CHA KOBE BRYANT CHAACHA SIMANZI