Home news BAADA YA ‘KUICHINJA’ SIMBA….KIIZA KWA KUJIAMINI AIBUKA NA HILI KUHUSU MABEKI WA...

BAADA YA ‘KUICHINJA’ SIMBA….KIIZA KWA KUJIAMINI AIBUKA NA HILI KUHUSU MABEKI WA SIMBA…


Baada ya kupeleka msiba mzito katika mitaa ya msimbazi, mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Burundi Hamis Kizza anayekipiga katika klabu ya Kagera Sugar amefunguka mambo mazito juu ya walinzi wa klabu ya Simba Sc Hennock Inonga pamoja na Joash Onyango.

Hamis Kizza alikua ni nyota wa mchezo wa jana ambao Kagera Sugar walipata ushindi wa goli moja kwa sifuri dhidi ya klabu ya Simba Sc katika dimba la Kaitaba. Kizza ndiye aliyetenganisha matokeo katika mchezo huo baada ya kufunga goli safi na pekee kwa upande wa Kagera Sugar ambao walikua katika uwanja wao wa nyumbani.

Baada ya mchezo huo kumalizika Hamis Kizza alipata nafasi ya kufanya mahojiano na waandishi wa ambao walijitokeza kushuhudia mchezo huo ambao ulikua ni mgumu kwa timu zote mbili. Kizza katika mazungumzo yake aligusia uwezo na kiwango cha walinzi wa klabu ya Simba Sc ambao ni Inonga na Onyango.

Kizza ameweka wazi kwamba walinzi hao ni wachezaji wazuri na imara sana licha ya kwamba alifanikiwa kufunga goli moja dhidi yao. Kizza amesema kwamba alitumia akili nyingi kuwatoroka kabla ya kufunga goli lake lakini hii haifanyi kuona kwamba Inonga na Onyango ni wachezaji wa kawaida sana.

Kizza ni mchezaji mkongwe ndani ya ligi kuu Tanzania bara ambapo miaka kadhaa ya nyuma nyota huyu aliwahi kupita katika vilabu vya Simba Sc na Yanga katika nyakati tofauti tofauti. Kizza kwa bahati nzuri sana ameweza kucheza kwa mafanikio makubwa sana akiwa na timu zote mbili na hivyo basi mashabiki wa Simba Sc na Yanga wamekua na kumbukumbu nzuri juu ya nyota huyu.

Kizza ni mshambuliaji hatari sana na mpaka sasa akiwa na Kagera Sugar tayari amefunga magoli mawili ikiwa ndio kwanza amejiunga na timu hii siku chache zilizopita. Kagera Sugar wamepata mshambuliaji mzuri na hatari sana ambaye anaweza kuwasaidia kufanya vizuri msimu huu ikiwa ni pamoja na kumaliza katika nafasi za juu katika msimamo wa NBC Premier League.

SOMA NA HII  DAKIKA CHACHE KABLA YA SIMBA vs YANGA..IBENGE AFUMBA MACHO AIPA USHINID TIMU HII....