Home Uncategorized CHIRWA ABEBESHWA BONGE MOJA YA ZIGO HUKO AZAM FC

CHIRWA ABEBESHWA BONGE MOJA YA ZIGO HUKO AZAM FC

UONGOZI wa Azam FC, umempa zigo kubwa mshambuliaji wao namba moja , Obrey Chirwa kuiongoza timu yake kufikia malengo ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara ulio mikononi mwa Simba.
Chirwa ametupia jumla ya mabao saba ndani ya ligi na ametoa jumla ya pasi tatu za mabao kesho ataingoza tena timu yake kumenyana na Polisi Tanzania Uwanja wa Uhuru.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Idd Cheche, Kocha Msaidizi wa azam FC alisema kuwa ili kuzipata pointi tatu ni lazima kufunga mabao mengi jambo ambalo lipo chini ya safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Chirwa pamoja na wachezaji wengine wote.
“Suala la pointi tatu lipo wazi halipatikani bila kufunga, safu ya ushambuliaji imekuwa na tatizo la kutumia nafasi tunazozipata hivyo tumewaambia kazi yao ni kufunga mabao yatakayotufanya tufikie malengo yetu ya kutwaa ubingwa wa ligi,” alisema Cheche.
SOMA NA HII  BREAKING: LIGI KUREJEA JUNI MOSI