Home Uncategorized BREAKING: LIGI KUREJEA JUNI MOSI

BREAKING: LIGI KUREJEA JUNI MOSI


JOHN Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa masuala ya michezo ikiwa ni pamoja na Ligi Kuu Tanzania Bara ni ruksa kuchezwa kuanzia Juni Mosi 2020.

  Magufuli amesema sasa michezo ni ruhusa kuendelea kuanzia Juni Mosi ikiwa ni pamoja na Ligi Kuu Bara, daraja la Kwanza na mingine. Pia michezo ya majeshi, mambo ya sanaa.

Suala la mashabiki uwanjani ameliacha kwa Wizara ya Afya.

Mbali na  michezo Rais Magufuli ameruhusu kufunguliwa kwa vyuo na wale wa kidato cha sita huku akiwataka wa shule ya msingi kusubiri kwanza.


Masuala yote ya mijumuiko isiyo ya lazima ilisimamishwa Machi 17 kutokana na Janga la Virusi vya Corona ambapo kwa sasa Serikali imesema kuwa hali ni shwari nchini.

SOMA NA HII  MANCHESTER UNITED WAMALIZA TOP 4,KUCHEZA LIGI YA MABINGWA ULAYA