Home Simba SC GOMES KUBADILI KIKOSI LEO, MKUDE NA MORRISON WAPEWA NAFASI

GOMES KUBADILI KIKOSI LEO, MKUDE NA MORRISON WAPEWA NAFASI

DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kuelekea mchezo wa leo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Mkapa atabadili kikosi cha ushindi.

Gomes ametoka kuongoza kikosi hicho kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi ikiwa dhidi ya Al Merrikh na aliambulia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90.

Kocha huyo amesema kuwa atawapa mapumziko baadhi ya wachezaji ambao walianza kwenye mechi yao hiyo iliyochezwa Machi 6, Uwanja wa Al Hilal.

Lengo la kufanya hivyo ni kuweza kuwapa muda wachezaji wake kwa ajili ya mchezo wao wa pili dhidi ya Al Merrikh unaotarajiwa kuchezwa Machi 16, Uwanja wa Mkapa.

“Utakuwa ni mchezo mgumu dhidi ya Prisons ila malengo yetu ni kuona kwamba timu inapata ushindi na kukusanya pointi tatu muhimu.

“Wachezaji wengine watapata muda wa kupumzika hii ni kwa ajili kuwapa nafasi wale wengine ambao hawakupata nafasi kwenye mchezo uliopita,” amesema.

Miongoni mwa wachezaji ambao wanapewa nafasi ya kuanza leo ni pamoja na kiungo mshambuliaji, Bernard Morrison,Ibrahim Ajibu, kiungo mkabaji Jonas Mkude na Said Ndemla.

SOMA NA HII  MKUTANO MKUU SIMBA:..OFISI ZA SIMBA KARIAKOO KUBADILISHWA..KWA MWAKA ZITAINGIZA TSH 500 MLN ..